Skip to main content

Posts

Samehe usamehewe

Uhondo wa Sanaa ya Ushairi na Kevin Wamalwa: Samehe usamehewe
Recent posts

Samehe usamehewe

Hayupo mja duniani asiyekosa asilani wala asitake samahani na imani ya mwenziwe Awe ndugu awe dada, au mwana.. Basi… kama hayupo asiyekosa akaitaka ghufira madhambiye kuondowa na , kwonewa imani na rehema, akawekwe huru nafsiye awe baba au mamaye binti au rafiki Basi, kwake kusahe ni faradhi mja mwene ila, samehe usamehewe Mlokole Mlumbi

Kukrani!

Shukrani! Shukrani zangu jazila, kwa chama cha NCOLTCL (nikotiko) Akawajazi jaala, kwa kutupa mualiko Tumeteremea kulla, tulosoma toka kwako Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Sikomi kuwahongera, walimu walofundisha walivyojifunga nira, ya maarifa kutupasha Tuzijenge mbinu bora, Kiswahili kufundisha Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Mambo hayo ni muhimu, mlotupasha uchao Mliyeshusha magumu, ya nadharia zao Tuboreke walimu, kwa wale tufudnishao Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Hongera mwalimu Kiarie, kwa kuonyesha mifano Lisanza nikusifie, kwazo sifa nono nono Alwiya zikufikie, ulivyokuwa mfano Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Sikusahau Atonia, kwa wako ukakamavu, Jinsi ulokakania, pasi kuonya ochovu Uneemee dunia, kwa kutupa wangavu Sasa tumeshalimuka, na mbinu za kufundisha Wanafunzi mlofika, shukrani nyingi sana Kwenu kuwa washirika, na mwiya wenu kupana Na sisi tukazoeka, na vipindi vil

Wangu Laazizi!

Wangu Laazizi Ulivyojisabilia, kwangu pasi samahani, Hujakosa kuniwia, radhi nili makosani, na skomi kujivunia, kuwa nawe maishani Mbuya wangu laazizi   Rahimu kanijalia, uwe wangu wa ubani, kito nisichokilalia, kwangu ili hisani Mola kaniumbia, uwe wangu muhisani, Mbuya wangu   laazizi Mara nikikuwaza, nyemi hinija moyoni, nafsi   hukaramukia, ninapokutia matoni pamwe nawe sjajutia, wala nsaili kwa nini Mbuya wangu laazizi   Na wajapotuchimbia, bado hatubandukani, Mawi walotutakia, na tabu zilosakini Yao hukuyasikia, ila uliniamini Mbuya wangu laazizi Mangapi umepitia, kunipenda maskini Lufufu mevumilia, huba letu kudhamini Vya mwiku umejilia, ukinipa na tumaini Mbuya wangu laazizi! Amwali hijitakia, ela uweja fulani Wala raha kupania, kuishi utukufuni Sakafu lijilalia, kusimisutu laini, Mbuya wangu Laazizi!   Pukute ulijilia, hukukimwa majani Sima ulibugia, mchana hata jioni Chai kavu

Kenya Itakuwepo

Niskize kote mlipo, niwape huno ujuzi Siku ya kura ijapo, ‘kiteuwa viongozi Kabila zetu zingapo, nyingi baidi ki’zazi Tutunze kenya iwepo, baada ya uchaguzi Na siasa tupigapo, tusitiye machokozi, kila mwahala twendapo, tudhihirishe wongozi, na wala sio matapo, ya kuzua machukizi, Hi' kenya itakuwapo, baada ya uchaguzi. Wazi mwajuwa malipo, ya kuzua uchafuzi, na kujifanya mapopo, tusiyatie maozi, ela yatendwe tulipo, wengi kawa wakimbizi, twataka kenya iwepo, baada ya uchaguzi kataa vidingapopo, vya kuzua uchochezi nao hawatakuwapo, tukichomana kwa mionzi wakipoa kwao pepo, nasi twazipiga kwenzi tuombe Kenya iwepo, baada ya uchaguzi Sisemi kupita hapo, menikaba usingizi, na chini nijilazapo, nawaasa wasikizi, kila mwahala mlipo, tusirudiye ya juzi, ili kenya ikawepo, baada ya uchaguzi. K.W Wamalwa Mlokole Mlumbi Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison
Hajafua Dafu Kama alivyo msasi, endaye kuwinda huwa Jenda kwa hamu na kasi,  kilenga kunasa njiwa Zimpatapo khasaisi, kumbe ndege hakutuwa Bado dafu hajafuwa, Mdavadi kijita Mesi Kwa makeke kahujuru, kuitafuta muruwa, Aionje hewa huru, kumbe nako  haikuwa Akapunjwa na Uhuru, alotaka kahiniwa Kabaki mechachamuwa,   zimwishiye furufuru Lisadiki sakumbimbi, walomlisha vongono  Kapotoshwa na wachimbi, na waja wasimaono Kamtowa kwenye kambi, alikopata usono Sasa yuasaga meno, akiulizwa haambi Kendea virambaramba, vichicha vya ukoloni Ndio navyo yuagamba, kuwa farasi mbioni Ni kama guo la mtumba, ‘pambwe mwari arusini Hata hawiki mjini, KANU jogoo wa shamba Nakoma wasiniambe, wanitusi wajuao Nachelea wanichimbe, wan’dhuru vibarakao Ila n’metowa ujumbe, wamwindhe nahodha wao “Sijetuwa meli yao, kwenye kaburi chimbe K.W Wamalwa Mlokole Mlumbi Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison